Akizungumzia suala hilo, Waziri Althusmann amesema kuwa jimbo hilo ndilo litakalokuwa la kwanza nchini Ujerumani kufudisha masomo hayo ya Kiislamu katika ratiba zake za masomo. Masomo hayo yanafanyiwa majaribio hivi sasa katika shule 42 za jimbo hilo ambapo zaidi ya wanafunzi 2000 wanajumuishwa. Iwapo walimu wanaohitajika kufudisha masoma hayo watapatikana basi masomo hayo yatanza kufundishwa rasmi katika shule zote za jimbo hilo mwaka 2012.
Waziri Althusmann amesema kuwa mpango huo unatekelezwa kwa lengo la kuwajumuisha Waislamu katika jamii ya Ujerumani na kuwaelemisha wanafunzi wasiokuwa Waislamu mafundisho ya Kiislamu. Akitoa mchango wake kuhusiana na suala hilo Ali Ishan Unlu, mkuu wa muungano wa ushirikiano wa jimbo la Niedersachsen na bunge la Ujerumani ameeleza kufurahishwa kwake na mpango huo na kusisitiza kuwa utakuwa na athari nyingi nzuri.
Hata hivyo ameongeza kuwa utekelezaji wake unahitajia mambo mengi yakiwemo ya kuimarishwa miundombinu, jambo ambalo amesema litahitajia msaada na ushirikiano wa jumuiya za Kiislamu. Amesema serikali ya Ujerumani inakusudia kusimamia masomo ya Kiislamu katika shule, kuwafundisha walimu wa Kiislamu na pia maimamu wa misikiti katika hali ambayo kwa mtazamo wa wataalamu wa masuala ya Kiislamu mambo hayo yanapasa kuchunguzwa kando. 656618