Huku likiaashiria kuzinduliwa mchezo ulio dhidi ya Uislamu nchini Austria katika kukaribia kufanyika uchaguzi wa kieneo nchini humo, kundi hilo linalofuatilia masuala ya amani limelaani kitendo hicho na kusema kuwa badala ya kupigwa marufuku ujenzi wa minara na misikiti nchini Austria, majengo hayo ya ibada yanapaswa kuongezwa nchini.
Limesema Waislamu wanahitajia misikiti kwa ajili ya kutekeleza ibada zao na kwamba iwapo jambo hilo litaruhusiwa, basi Waislamu watahisi zaidi kuwa sehemu ya jamii ya nchi hiyo.
Taarifa hiyo imesema katika sehemu nyingine kwamba, demokrasia ya Magharibi pia inajumuisha uhuru wa kuabudu na kwamba maana ye neno hilo katika jamii haipaswi kubanwa. 656647