Makari 140 kutoka nchi 73 watashiriki katika mashindano hayo katika nyanja za kuhifadhi Qur'ani nzima na kusoma kitabu hicho.
Mkuu wa kitengo cha Qur'ani cha Idara ya Wakfu na Masuala ya Zaka cha Libya ambayo ndiyo inayosimamia mashindano hayo amesema yataendelea hadi tarehe 26 Septemba.
Amesema kuwa kutakuwepo ratiba mbalimbali za kiutamaduni na kidini pambizoni mwa mashindano hayo na kwamba wasomi na maulamaa kutoka nchi mbalimbali watahutubia katika misikiti ya Libya wakizungumzia masuala mbalimbali.
Ratiba nyingine ya mashindano hayo ni maonyesho ya vitabu vya kidini na makongamano ya masuala ya utamaduni na dini. 656842