IQNA

Rehal ya mbao ya Msahafu katika Makumbusho ya Haram ya Hadhrat Abbas (AS)

18:55 - June 16, 2026
Habari ID: 3482367
Rehal ya mbao
IQNA – Makumbusho ya Hazina na Miswada ya Al‑Kafeel, yaliyo ndani ya Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas (AS) mjini Karbala, yameweka hadharani Rehal ya mbao ya Msahafu iliyotegenezwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Al‑Kafeel, Rehal ya mbao ya Msahafu iliyopambwa kwa mbinu ya Khatam‑Kari (Marquetry) ina uzito wa gramu 1,155 na kimepambwa kwa michoro ya Kiislamu yenye kuvutia.

Kazi hiyo inaonesha michoro ya maua na maumbo ya kijiometri ya Khatam‑Kari iliyochongwa kwa ustadi sambamba na nakshi za Kiislamu, ikiakisi umakini, umaridadi na upekee wa sanaa za mapambo katika ustaarabu wa Kiislamu.

Rehal hii inadhihirisha ustadi wa mafundi katika kuunganisha vipengele vya mapambo ndani ya kazi za mbao, kwa kuzingatia matumizi yake ya kivitendo, kuiweka Qur’ani Tukufu wakati wa tilawa, na wakati huohuo kuipa thamani ya kisanii inayokifanya kuwa na mvuto wa kipekee wa kimaumbo.

Makumbusho ya Hazina na Miswada ya Al‑Kafeel yanaendelea na juhudi zake za kuhifadhi na kuonesha turathi na athari za kihistoria, hatua inayodhihirisha utajiri na utofauti wa sanaa za Kiislamu, pamoja na kuchangia kuinua uelewa wa thamani yake ya kisanii na kitamaduni miongoni mwa wageni na watafiti.

3497856

captcha