Hafla hiyo, iliyofanyika kwa kumbukumbu ya tarehe 10 Muharram, ilihudhuriwa na idadi kubwa ya waombolezaji na wapenzi wa Imam Hussein (AS).
Kwa mujibu wa taarifa ya Al-Ahed News, hafla hiyo ilianza asubuhi ya Ijumaa kwenye kaburi la shahidi Nasrallah lililoko katika viunga vya kusini mwa Beirut.
Picha zilizochapishwa kutoka hafla hiyo zinaonesha umati mkubwa wa wapenzi wa Ahlul-Bayt (AS) waliokusanyika mahali hapo kuomboleza siku ya Ashura.
Washiriki wa hafla hiyo walisisitiza tena kushikamana kwao na misingi ya harakati ya Ashura, pamoja na utamaduni wa kujitoa muhanga na muqawama.
Hafla hiyo ilifanyika katika mazingira yaliyogubikwa na huzuni na majonzi, huku waombolezaji wakipaza sauti za nadha na kaulimbiu za Ashura na muqawama.
Washiriki pia waliwatukuza mashahidi wa muqawama kwa kubeba bendera za Husseini pamoja na picha za shahidi Nasrallah.
Tarehe 10 Muharram, inayojulikana pia kama Ashura, ni siku yenye umuhimu mkubwa kwa Waislamu duniani kote. Siku hii huashiria kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (AS) pamoja na wenzake katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria sawa na 680 Miladia.
Kujitoa muhanga kwa Imam Hussein (AS) huendelea kukumbukwa na kuombolezwa na Waislamu hasa wa madhehebu ya Shia kote duniani.
3497977