Idadi kubwa ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq walisafiri hadi mji mtakatifu wa Karbala ili kushiriki katika majlisi na ibada za maombolezo ya kumbukumbu ya kuuliwa shahidi kwa Imam Hussein (AS).
Mwaka huu, mwezi wa Muharram kwa kalenda ya Hijria ya mwezi ulianza tarehe 17 Juni nchini Iraq, siku moja baada ya Iran; kwa hivyo, siku ya Ashura nchini humo imeangukia tarehe 26 Juni.
Makundi mengi ya waombolezaji yamehudhuria katika haram takatifu za Imam Hussein (AS) na Hazrat Abbas (AS) huko Karbala, kwa ajili ya kuomboleza na kutekeleza ibada na taratibu maalumu zinazofahamika sana nchini Iraq.
Tarehe 10 Muharram, inayojulikana pia kama Ashura, ni siku yenye nafasi kubwa kwa Waislamu duniani kote. Siku hii ni kumbukumbu ya kuuliwa shahidi kwa Imam Hussein (AS) pamoja na wenzake katika vita vya Karbala mwaka 61 Hijria Qamaria sawa na 680 Miladia.
Kujitoa muhanga kwa Imam Hussein (AS) huendelea kukumbukwa na kuombolezwa na Waislamu wa Kishia ulimwenguni kote.
349797