IQNA

Mtafiti wa Kishia akamatwa Bahrain baada ya kuandika kuhusu Ashura

15:21 - June 27, 2026
Habari ID: 3482408
IQNA – Ukiendelea na mnyororo wake wa kimfumo wa kuzuia uhuru wa maoni na kukandamiza wataalamu na watendaji wa kiraia, ufalme wa kiimla wa Bahrain umemkamata mtafifi mwelekeo wa Shia.

Maafisa wa utawala wa Al-Khalifa wamemkamata Bi. Fatima Haroun, ambaye ni mtafiti wa masuala ya kijamii, kufuatia maoni aliyoyatoa katika mtandao wa Instagram kuhusiana na tukio la Ashura.

Siku ya Alhamisi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain ilidai kuwa kukamatwa huko kumetokana na kile ilichokiita “matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii,” ikidai kuwa maudhui aliyoyachapisha yamevunjia heshima moja ya madhehebu ya Kiislamu.

Hata hivyo, Baraza la Masuala ya Wafungwa wa Bahrain limelaani vikali hatua hiyo ya kikatili, likibainisha kuwa ni mwendelezo wa mbinu za kimfumo za kuzima sauti za watu huru, kukandamiza wasomi, na kuingilia uhuru wa kifikra nchini humo.

Katika taarifa yake, Baraza hilo limeeleza kuwa tuhuma zinazomkabili Bi. Fatima Haroun ni zile za jumla na zisizo na msingi thabiti; mbinu ambayo imekuwa ikitumiwa mara kwa mara kama nyenzo ya kuwafunga midomo wakosoaji na kuhalalisha uhalifu wa kuua uhuru wa kujieleza.

Kwa mujibu wa Baraza hilo, hatua za mtafiti huyo hazikuwa kitu kingine isipokuwa ni utekelezaji wa haki yake ya msingi ya kutoa maoni.

Taarifa hiyo ilisisitiza kwa uzito kuwa kukamatwa kwa msomi na mwanaharakati mashuhuri wa kijamii kisa na maana ni kutoa maoni yake mtandaoni, ni kielelezo tosha cha kuongezeka kwa mashinikizo dhidi ya tabaka la wasomi na wenye weledi. Hii ni harakati ya makusudi ya kukandamiza mitandao ya kidijitali na kuimarisha udhibiti wa kiusalama juu ya uhuru wa kutoa maoni, hatua ambayo ni kinyume kabisa na mikataba pamoja na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.

3497981

Habari zinazohusiana
captcha