IQNA

Kuanza mashindano ya masomo ya Qur'ani kwa wanawake wa Qatar

17:04 - September 20, 2010
Habari ID: 1997540
Masomo maalumu ya Qur'ani kwa wanawake wa Qatar yameanza siku ya Jumamosi tarehe 18 Septemba na yamepangwa kuendelea hadi mwezi Februari mwakani.
Kwa mujibu wa gazeti la Qatar la as-Sharq masomo hayo yanadhaminiwa na kitengo cha wanawake cha shirika la huduma za kibinadamu la Raf la nchini Qatar na kupitia masomo hayo, wanawake wa Qatar watapata fursa ya kujifunza mafundisho ya Qur'ani kuhusiana na suala la malezi.
Masomo hayo ni sehemu ya ratiba ya shirika la Raf ya kuwapa wamawake masomo ya kimalezi na kielimu ili kuwajenga na kuwatayarisha kwa ajili ya kuwapa watoto wao malezi yanayofaa kwa msingi wa mafundisho ya Qur'ani na hadithi za Mtume Mtukufu (saw).
Wataalamu na washauri wa masuala ya sheria za Kiislamu wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar watashirikiana na shirika hilo katika kutoa mafunzo hayo. Vikao na ziara mbalimbali zitaandaliwa na shirika hilo ili kuwapa wanawake watakaoshiriki katika masomo hayo fursa ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii. 657774
captcha