Kwa mujibu wa tovuti ya al-Iraq Liljamee' kikao hicho kinawashirikisha wawakilishi wa taasisi na jumuiya mbalimbali za Kiislamu za Marekani ambao wanajadili na kubadilishana mawazo kuhusiana na ujenzi wa kituo na msikiti huo karibu na sehemu iliyotokea mashambulio ya kigaidi ya Septema 11 mwaka 2001 mjini New York. Kuongezeka vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na kuchomwa Qur'ani Tukufu kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mashambulio hayo ni baadhi ya mambo yatakayojadiliwa katika kikao hicho. Akizungumzia suala hilo, Sheikh Ubeid, mkuu wa Baraza la Uongozi wa Kiislamu la mjini New York, baraza ambalo ni moja ya jumuiya muhimu zinazoandaa kikao hicho amesema kuwa, baadhi ya viongozi wa Marekani ambao huko nyuma walikuwa na wasiwasi na woga mkubwa wa kuunga mkono ujenzi wa msikiti na kituo hicho cha Kiislamu katika sehemu iliyotajwa hii leo wamebadilika na kuwa waungaji mkono wakubwa wa mradi huo.
Wawakilishi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Marekani Kaskazini, Idara ya Kiislamu ya Marekani Kaskazini, Muungano wa Kiislamu wa Marekani Kaskazini na Baraza la Uhusiano wa Kiislamu na Marekani ni miongoni mwa wawakilishi wa jumuiya muhimu zinazoshiriki katika kikao hicho. 658708