IQNA

Vikao vya tafsiri ya Surat al-Hujurat kufanyika mjini Manchester

17:13 - September 20, 2010
Habari ID: 1997584
Vikao vya muda mfupi vya kufasiriwa Surat al-Hujurat vitafanyika katika Kituo cha Vijana wa Kiislamu mjini Manchester (MYF) Uingereza kuanzia Jumamosi tarehe 16 0ktoba.
Kwa mujibu wa tovuti ya IIDR, vikao hivyo vya tafsiri ya Surat al-Hujurat ambavyo vimeandaliwa na Chuo cha Utafiti wa Qur'ani cha Uingereza BAQS, vitakuwa vikianza saa tatu asubuhi na kuendelea hadi sa sita na nusu adhuhuri.
Majukumu na tabia za mwanadamu mkabala na Mwenyezi Mungu, Mtume Mtukufu (saw), Waislamu wenzake na jamii anayoishi ni baadhi ya mambo yatakayojadiliwa katika kufasiri sura hiyo. Masuala mengine yatakayojadiliwa kwa kutegemea tafsiri mbalimbali za sura hiyo ni pamoja na udharura wa kujitakasa Muislamu, nguzo za jamii ya kisasa ya Kiislamu na lengo la kubuniwa mfumo wa jamii ya Kiislamu.
Chuo cha Utafiti wa Qur'ani cha Uingereza huandaa vikao vya tafsiri za sura tofauti za Qur'ani katika miji mbalimbali ya nchi hiyo. 658721
captcha