IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu kufanyika Afrika Kusini

17:48 - September 20, 2010
Habari ID: 1997959
Mashindano ya taifa ya kusoma Qur'ani Tukufu yatafanyika tarehe 24 hadi 26 za mwezi huu wa Septemba katika mji wa Cape Town huko Afrika Kusini.
Mashindano hayo yatasimamiwa na Taasisi ya Qur'ani ya Afrika Kusini (SAQU) ikishirikiana na msikiti wa al Karim wa Cape Town.
Mashindano hayo ya wanaume watafanyika katika ngazi za watoto, vijana na watu wazima.
Mashindano ya awali ya watoto yataanza tarehe 24 Septemba na ya vijana na watu wazima yatafanyika siku moja baadaye. Washindi katika mashindano hayo ya awali watachuana katika fainali ya mashindano hayo tarehe 26 Septemba.
Mashindano hayo yatafanyika kwa lengo la kuwaenzi walimu wa Qur'ani Tukufu, kupandisha juu kiwango cha elimu ya Qur'ani na kulea wasomaji wa kimataifa.
Taasisi ya Qur'ani ya Afrika Kusini ni jumuiya isiyokuwa ya serikali iliyoasisiwa kwa shabaha ya kueneza taaluma ya Qur'ani na kutayarisha uwanja mzuri wa mawasiliano zaidi kati ya taasisi zinazoshughulikia masuala ya Qur'ani, wasomaji, wanafikra na mahifafidhi wa kitabu hicho nchini humo. 658949
captcha