IQNA

Njama ya kuivunjia heshima Qu'ani huko Marekani ilipangwa huko nyuma

12:20 - September 21, 2010
Habari ID: 1998457
Tukio la kuvunjiwa heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani nchini Marekani si jambo lililoanzishwa na kasisi wa kanisa dogo tu la Marekani bali ni njama kabambe iliyopingwa tokea huko nyuma.
Hayo yamesemwa na Nabii Maknun mtarjumi wa vitabu vya Imam Khomeini kwa lugha ya Amharic na mhariri mkuu wa jarida lenye wasomaji wengi nchini Ethiopia la Addis Admass katika mahojiano yake na shirika la IQNA. Amesema kuwa tukio hilo ni njama iliyopangwa na maadui wa Uislamu na masuala ya kiroho duniani. Amesema, kama tulivyoona njama hiyo kwanza ulizunduliwa na kasisi mmoja ambaye baadaye alitupilia mbali mpango wake kisha wimbi la kukivunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani likaanza kuenea katika maeneo mbalimbali duniani.
Mhariri wa jarida la kila wiki la Addis Admass amesema tendo hilo la kuvunjiwa heshima kitabu cha Mwenyezi Mungu halitaishia kwenye Qur'ani tu bali tokea sasa vitabu vingine vitakatifu vitavunjiwa heshima hadi pale Waislamu na wafuasi wa dini nyingine kote duniani watakaposhirikiana na kubuni njia za kivitendo za kukabiliana na vitendo hivyo viovu. 659554


captcha