Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zimehudhuriwa na maulama, wanafikra wa ulimwengu wa Kiislamu na viongozi wa kieneo wa Libya.
Washindani 140 kutoka nchi 73 wanachuana katika mashindano hayo yanayosimamiwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Zaka ya Libya. Mashindano hayo yanafanyika katika nyanja za kuhifadhi Qur'ani na tajwidi.
Mashindano hayo yataendelea hadi tarehe 26 Septemba na yataandamana na ratiba mbalimbali za kidini.
Vilevile wanazuoni na walinganiaji wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali walioalikwa na Wizara ya Wakfu ya Libya watahutubia vikao mbalimbali kuhusu maudhui tofauti.
Pambizoni mwa mashindano hayo ya Qur'ani tuzo ya al Fatih, kunafanyika maonyesho ya vitabu vya kidini. 659571