Mradi wa kujenga Bustani ya Itikadi ulianza kutekelezwa siku ya Jumatatu tarehe 20 katika mji wa Mardin nchini Uturuki. Mradi huo unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Utamaduni na Utalii ya Uturuki na ofisi ya meya wa Mardin utawawezesha Waislamu na Wakristo kukutana na kujadiliana huko kuhusiana na masuala ya itikadi zao baada ya kutekeleza ibada zao kwenye misikiti na makanisani.