IQNA

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Brunei kuandaa maonyesho ya kaligrafia ya Kiislamu

12:15 - September 22, 2010
Habari ID: 1999266
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha nchini Brunei kinaandaa maonyesho ya kaligrafia ya Kiislamu tokea siku ya Jumatatu tarehe 20 Septemba.
Kwa mujibu wa tovuti ya Brudirect, maonyesho hayo ambayo yanafanyika pambizoni mwa tamasha la wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha Brunei yataendelea kwa muda wa wiki moja. Licha ya hayo, kongamano la mafundisho ya kaligrafia ya Kiislamu na mashindano ya ipigaji picha wa kaligrafia ya Kiislamu pia yatafanyika katika kipindi chote cha kufanyika tamasha hilo.
Makongamano ya usomaji Qur'ani na kaligrafia ya dijitali ya Kislamu pia yatafanyika katika tamasha hilo. 660075
captcha