IQNA

Mpango wa uchapishaji na tarjumi ya Qur'ani kutekelezwa nchini Kuwait

12:29 - September 22, 2010
Habari ID: 1999270
Kamati ya Uarifishaji Uislamu ya Kuwait imetangaza habari ya kutekelezwa mpango wa uchapishaji na kutarjumu Qur'ani Tukufu kwa lugha mbalimbali nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Kuwait KUNA, Jamal as-Shati, naibu katibu mkuu wa kamati hiyo amesema kuwa mafundisho yenye thamani kubwa ya Qur'ani Tukufu ni sababu muhimu zaidi inayowapelekea watu wasiokuwa Waislamu kusilimu na kuukubali Uislamu.
Kwa msingi huo amesema kuwa kamati hiyo ina mpango wa kutarjumi kitabu hicho kitakatifu katika lugha hai 14 za dunia zikiwemo za Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kijerumani, Kichina, Kifilipino na Kibosnia.
Mwishoni mwa matamshi yake as-Shati amesisitiza udharura wa kuenezwa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Waislamu na wasio Waislamu na kuongeza kuwa kamati ya kuuarifisha Uislamu ya Kuwait ina mpango wa kuchapisha na kugawa nuskha laki moja za Qur'ani miongoni mwa watu, bei ya kila nuskha ikiwa ni dinari mbili za Kuwait. 660206
captcha