IQNA

Kumbukumbu ya maombolezo ya Imam Swadiq (as) kufanyika mjini London

12:23 - September 22, 2010
Habari ID: 1999277
Makumbusho ya kuuawa shahidi Imam Ja'far Swadiq (as) yamepangwa kufanyika tarehe 2 Oktoba katika Kituo cha Kiislamu mjini London Uingereza.
Makumbusho hayo yataanza saa kumi na moja alasiri na kuendelea kwa muda wa masaa mawili katika kituo hicho. Katika makumbusho hayo, Hujjatul Islam wal Muslimeen Ahmad Huneif, mwanazuoni raia wa Canada ambaye alipata mafunzo yake ya kidini katika Chuo cha Kidini cha Qum nchini Iran atazungumzia maisha na sifa za Imam huyo wa sita wa madhebu ya Shia.
Makumbusho hayo ambayo yatahudhuriwa na idadi kubwa ya Waislamu wanaoishi nchini Uingereza, yatamalizika kwa kuswaliwa swala ya jamaa ya Maghrib. 660450
captcha