Kituo cha Medya73 kimeripoti kuwa mkusanyiko huo utakaosimamiwa na Jumuiya ya Wapenzi wa Mtume wa Uislamu unafanyika kwa shabaha ya kupinga vitendo vya kuchomwa moto Qur'ani nchini Marekani na kuvunjiwa heshima neno tukufu la Mwenyezi Mungu.
Msemaji wa Jumuiya ya Wapenzi wa Mtume wa Uislamu Ali Ortaç amesema kuwa siku chache zilizopita tulishuhudia kitabu cha Mwenyezi Mungu kikichomwa moto katika nchi za Marekani na Australia kwa kisingizio cha mashambulizi ya Septemba 11, na vilevile Mayahudi wenye misimamo ya kufurutu mipaka katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu wamekichana na kukirarua kitabu hicho kitukufu. Ali Ortaç amewataka wapenzi wa dini ya Kiislamu katika mkoa wa Batman kukusanyika katika medani kuu ya mji huo Jumapili ijayo kwa shabaha ya kulaani vitendo hivyo vichafu.
Ali Ortaç vilevile amewataka washiriki wote wa kike na kiume kubeba Qur'ani katika mkusanyiko huo na kupinga kitendo cha kudharauliwa Qur'ani Tukufu kwa kuonyesha mapenzi yao ka muujiza huo wa Mtume Muhammad (saw). 660566