Martin Peretz amekuwa akichapisha makala zinazovunjia heshima Uislamu na Waislamu na kutengwa kiti cha chuo kikuu cha jina lake kumewakasirisha mno wanafunzi na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Harvard wanaopinga mitazamo ya kibaguzi.
Kitengo hicho cha utafiti ambacho kitagharimu dola laki tano kitafunguliwa Ijumaa ya tarehe 24 Septemba lakini inaonekana kuwa mpango huo huenda ukaahirishwa kutokana na malalamiko makubwa ya wanafunzi wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Harvard.
Stephan Walt afisa uhusiano wa kimataifa wa Chuo Kikuu cha Harvard amesema kuwa matamshi yanayotolewa na Martin Peretz kuhusu Waislamu yanasikitisha mno na iwapo angetoa matamshi kama hayo kuhusu Mayahudi au Waafrika hapana shaka yangesababisha mvutano mkubwa nchini.
Wakati huo huo wanachuo wa Chuo Kikuu cha Harvard wamewaandikia barua viongozi wa chuo hicho wakitaja mpango wa kuanzisha kitengo cha Martin Peretz kuwa ni kutetea misimamo ya kibaguzi na wametoa wito wa kusimamishwa mpango huo.
Katika matamshi yake ya hivi karibuni, Martin Peretz alisema kuwa nafsi na maisha ya Waislamu hayana thamani yoyote akidai kuwa Waislamu wanastahiki kubaguliwa. 660640