Kasisi al Anba Bishoy Katibu wa Jumuiya Takatifu ya Kikristo ya Misri ametoa wito wa kufutwa baadhi ya aya za Qur'ani ambazo amedai zinapingana na itikadi za Kikristo, jambo ambalo limekabiliwa na upunzani mkali wa maulama na wanafikra wa al Azhar hususan Sheikh wa taasisi hiyo ya juu zaidi ya kidini nchini Misri.
Ripoti zinasema kwamba Sheikh wa al Azhar atatoa taarifa hii leo Jumamosi akijibu matamshi ya Kasisi Bishoy.
Katika upande mwingine Naibu Mkuu wa Masuala ya Ulinganiaji wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Misri Salim Abdul Jalil amekosoa matamshi hayo ya Kasisi Bishoy na kusisitiza kuwa itikadi za Waislamu ni mstari mwekundu ambao wasokuwa Waislamu hawaruhusiwi kutoa maoni juu yake.
Kasisi huyo wa Kikristo alidai katika kongamano lililofanyika hivi karibuni huko Cyprus kwamba moja ya aya za kitabu kitakatifu cha Qur'ani ilibiniwa katika kipindi cha khalifa wa tatu Othmani bin Affan baada ya kufariki dunia Mtume Muhammad (saw) na kwamba aya hiyo inapingana na itikadi za Kikristo.
Hata hivyo baada ya kukabiliwa na malalamiko makubwa, kasisi hiyo ametangaza kuwa hakuwa na nia ya kuuvunjia heshima Uislamu na matukufu yake na kwamba maneno yake yameeleweka visivyo. 661828