Wakili huyo amedai kwamba kanali za televisheni za Waislamu wa Kishia kama al Anwar na Fadak zimetengenga zehemu kubwa ya vipindi vyao kwa ajili ya kuvunjia heshima itikadi za Waislamu wa Kisuni!
Sehemu moja ya mashtaka hayo yaliyowasilishwa mahakamani inasema: "Kuendelea kurushwa matangazo ya televisheni za Waislamu wa Kishia katika satalaiti ya Nale Sat inayomilikiwa na serikali ya Misri kunapingana na katiba ya nchi hiyo, kwani katiba hiyo inasisitiza juu ya uhuru wa itikadi na kuheshimiwa dini.
Wakili huyo ametoa madai hayo akisahau kwamba hii leo Waislamu wa madhehebu ya Shia katika nchi za Misri na Saudi Arabia wananyimwa haki zao za kimsingi za kiraia ikiwa ni pamoja na uhuru wa kutekeleza ibada.
Habari zinasema kuwa hatua ya kanali za televisheni za Waislamu wa Kishia ya kufichua sura halisi ya Mawahabi na itikadi zao potofu ndiyo sababu ya mashinikizo ya kundi hilo la Mawahabi dhidi ya satalaiti ya Nile Sat yanayoitaka isimamishe matangazo ya televisheni za Waislamu wa Kishia. 662900