IQNA

Kongamano la Uislamu na Waislamu kufanyika Chicago

15:37 - September 27, 2010
Habari ID: 2002531
Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC ikishirikiana na Chuo cha Kiislamu cha Marekani zinapanga kuitisha kongamano la Uislamu na Waislamu ambalo litajadili masuala ya Waislamu nchini Marekani. Kongamano hilo limepangwa kufanyika tarehe 28 hadi 30 Septemba.
Miongoni mwa malengo ya kongamano hilo ni kuchunguza masuala ya Waislamu wa Marekani, kutafuta njia za kutatua matatizo yao, kiwango cha ushirikiano wa OIC na Waislamu wanaoishi Marekani na kuanzisha ushirikiano mpana zaidi kati ya jumuiya ya OIC na jumuiya za Waislamu wa Marekani.
Kongamano hilo litafunguliwa na hotuba ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC Ekmeleddin Ihsanoglu na kuhutubiwa na wasomi kadhaa wa Marekani.
Bwana Ihsanoglu pia atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa jamii ya Kiislamu ya Marekani na kuchunguza matatizo yanayowakabili. 663986
captcha