IQNA

Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia:

Kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu hakuwezi kusamehewa

14:55 - September 28, 2010
Habari ID: 2003239
Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia amesema kuwa serikali ya nchi hiyo haitanyamazia kimya kitendo chochote kinachovunjia heshima dini ya Kiislamu na itazuia vitendo kama hivyo.
Mashitah Ibrahim amesisitiza kuwa vitendo vinavyovunjia heshima dini ya Kiislamu haviwezi kusamehewa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Barnama, Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia amesisitiza kuwa dharau ya aina yoyote dhidi ya matukufu ya Kiislamu haitasamehewa na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya vitendo kama hivyo.
Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia ambaye ametoa matamshi hayo kufuatia kitendo cha kasisi mmoja wa Kikristo cha kuweka mkanda wa video unaokashifu Uislamu katika ukurasa wa mtandao wa YouTube, ameongeza kuwa iwapo hatua kali hazitachukuliwa, watu wanaovunjia heshima matukufu ya Kiislamu wataendeleza mwenendo huo.
Mashitah bint Ibrahim ameelezea kusikitishwa mno na hatua hiyo na kuwataka viongozi wa serikali ya Malaysia kushughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.
Gazeti moja la Malaysia limeripoti kuwa mkuu wa muungano wa waandishi weblogu wa Kiislamu wa Malaysia Zainul Abidin amesema kuwa Kasisi Benjamin Stephan wa kanisa la Sarawak ameweka mkanda wa video unaovunjia heshima Uislamu katika mtandao wa YouTube. 664473
captcha