Kikao hicho ambacho kimeandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu na Chuo cha Kiislamu cha Marekani kina lengo la kuchunguza masuala ya Waislamu nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la Arab News, masuala ya Waislamu wanaoishi nchini Marekani, njia za kutatua matatizo yao, kiwango cha ushirikiano wa OIC na Waislamu wa Marekani na njia za kuimarisha ushirikiano wa OIC na jumuiya za Kiislamu za Marekani ni mambo mengine yatakayojadiliwa.
Kikao hicho kimefunguliwa kwa hotuba ya Ekmeleddin Ihsanoglu Katibu Mkuu wa OIC na kisha kufuatiwa na hotuba za John Esposito, mhadhiri wa masuala ya kidini na kimataifa na utafiti wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Georgetown, Swafa Zarzour, mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Amerika Kaskazini na Abdul Hamid Jackson, mhadhiri wa utafiti wa Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Michigan.
Msanii mashuhuri Sami Yusuf atawatumbuiza washiriki wa kikao hicho hapo kesho adhuhuri Jumatano. 663986