IQNA

Uislamu na changamoto za karne ya 21 kuchunguzwa mjini Kuala Lumpur

15:02 - September 28, 2010
Habari ID: 2003247
Kikao cha kimataifa cha kuchunguza Uislamu na changamoto za karne ya 21 kimepangwa kufanyika tarehe 8 Oktoba katika Kituo cha Masomo ya Juu ya Kiislamu cha Malaysia IAIS huko mjini Kuala Lumpur.
Kwa mujibu wa tovuti ya kituo hicho, mmoja wa shakhsia muhimu watakaohutubia katika kikao hicho ni Sheikh Ahmad Badru Deen Hassoun, Mufti Mkuu wa Syria.
Mambo yatakayojadiliwa katika kikao hicho yatatangazwa na kutarjumiwa kwa lugha kadhaa kikiwemo Kiingereza. 664014
captcha