IQNA

Katuni zinazovunjia heshima Uislamu kuchapishwa kama kitabu!

15:49 - September 28, 2010
Habari ID: 2003296
Katika hali ambayo ulimwewengu wa Kiislamu ungali katika hasira kubwa ya kuvunjiwa heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani nchini Marekani, afisa mmoja wa gazeti la Denmark ambalo miaka mitano iliyopita lilichapisha vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) ametangaza kuwa ana nia ya kuchapisha kitabu kinachokusanya vibonzo hivyo.
Flemming Rose wa gazeti la Jyllands-Posten ametangaza kuwa atazindua kitabu hicho alichokipa jila la "The Tyranny of Silence" hapo tarehe 30 Septemba kwa mnasaba wa kutimia miaka mitano tangu kuchapishwa kwa mara ya kwanza vibonzo hivyo.
Licha ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark kupinga suala la kuchapishwa kitabu hicho lakini afisa wa gazeti la Jyllands-Posten Flemming Rose anasisitiza kuwa atatumia haki yake ya uhuru wa kueleza fikra na kuchapisha kitabu hicho kinachovunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark pia imezitaka ofisa za balozi wa nchi hiyo katika nchi za Kiislamu kutoonyesha radiamali yoyote mbele ya maandamano ya Waislamu na kutojibu maswali ya waandishi wa habari. 664675


captcha