Watu hao wasiojulikana walikuwa na nia ya kuchoma moto msikiti huo kwa kutupa mada za milipuko ndani ya eneo hilo la ibada lakini hawakufanikiwa.
Polisi ya Uholanzi waliofikia msikitini hapo wamesema kuwa shambulizi hilo halikusababisha madhara na kwamba maneno yanayopinga Uislamu yameandika katika kuta zake.
Polisi na Uholanzi pia imeimarisha usalama katika eneo hilo na tayari imeanza kuchunguza tukio hilo na kuwafuatilia watu waliohusika nalo.
Mwanzoni mwa mwezi uliopita kundi moja la wabaguzi lilivamia na kuchoma moto sehemu ya msikiti huo. Polisi na kikosi cha zima moto kilifanikiwa kuzima moto huo ambao haukusababisa hasara kubwa. 665363