IQNA

Mzungumzo katika kivuli cha ujenzi wa vitongoji ni kupoteza wakati

11:30 - September 30, 2010
Habari ID: 2004425
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina ni jambo hatari sana na kwamba kuendelea mazungumzo katika kivuli cha ujenzi wa vitongoji hivyo ni upotezaji wakati.
Akizungumza hivi karibuni na shirika la habari la Palestina Wafa, Amru Musa amesema kuwa Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina anatazamiwa kushiriki katika kikao cha Kamati ya Amani ya nchi za Kiarabu ambacho kinatazamiwa kufanyika Jumatatu ijayo na kuwashirikisha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo. Amesema kikao hicho kitachunguza njia za kumsaidia Abbas katika juhudi zake za kukabiliana na ujenzi wa vitongoji hivyo.
Musa amesema kikao hicho pia kitachunguza matukio magumu na nyeti ya mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Mahmoud Abbas na viongozi wa utawala haramu wa Israel. Amesikitishwa na msimamo wa Wazayuni wa kuendelea kujenga vitongoji vya walowezi katika ardhi ya Palestina kinyume na mapatano yaliyofikiwa huko nyuma ya kuakhirisha ujenzi huo ili kufanikisha mapatano ya pande mbili. Amesisitiza kuwa kuendelea mazungumzo hayo katika mazingira ya hivi sasa ya kuendelea kujengwa vitongoji ni kupoteza wakati tu na vilevile kuhatarisha maslahi ya Waarabu. 665562
captcha