Kwa mujibu wa tovuti ya Brudirect warsha hiyo inafanyika kwa madhumuni ya kuongeza maarifa na ujuzi wa wanachuo katika uwanja wa kaligrafia ya Kiislamu, kubadilishana uzoefu wa taaluma hiyo, kufahamu maana na utambulisho wa kaligrafia ya Kiislamu pamoja na historia fupi ya sanaa hiyo ya miaka 1400.
Karibu wanachuo 100 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na shule nyingine za Brunei wanashiriki katika warsha hiyo.
Mbali na kufundisha masomo ya kaligrafia, wawakilishi kutoka vituo vya historia ya Brunei na wito wa Kiislamu vya nchi hiyo wanaoshiriki katika warsha hiyo pia watatoa hotuba mbalimbali kuhusiana na suala la sanaa ya kaligrafia ya Kiislamu. 665663