IQNA

Kutiwa saini mkataba wa kulaani kila aina ya dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu

11:41 - October 02, 2010
Habari ID: 2005217
Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amemwandikia barua Nabih Berri, spika mwenzake wa Lebanon akitoa pendekezo la kubuniwa mkataba wa kimataifa wa kulaani kila aina ya dharau dhidi ya Qur'ani Tukufu na matukufu ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa gazeti la as-Safir la Lebanon, barua hiyo imekabidhiwa kwa Berri na Ghadhamfar Rukni Abadi, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Beirut.
Katika mazungumzo hayo, Spika wa Lebanon huku akilaani udhalilishaji wa Qur'ani amekaribisha pendekezo hilo la Larijani na kuzitaka serikali za Kiislamu kushirikiana katika kukabiliana na njama ya kuenezwa vitendo vya dharau, chuki na uadui dhidi ya Uislamu. 666526
captcha