Kwa mujibu wa televisheni ya Raswid, maombolezo hayo yataanza leo Jumapili alasiri katika Husseiniyyah ya Batul katika mji wa al-Awaamiyyah.
Sheikh Naji al-Ibadi atazungumza katika maombolezo hayo kuhusiana na maisha na shakhsiya ya Imam Swadiq (as).
Maombolezo mengine kama hayo pia yamepangwa kufanyika katika Husseiniya ya Abul Fadhl al-Abbas (as) katika mji wa Seihat ambapo Said al-Maatiq mmoja wa mahatibu na wahubiri mashuhuri wa Kishia nchini Saudia amepangiwa kuhutubu.
Maombolezo hayo yatatangazwa moja kwa moja kupitia mtandao wa intaneti kwa anwani ifuatayo: www.abolfadlalabss.com. 667241