Mashia wa Uturuki leo Jumatatu wameshiriki katika maombolezo ya kukumbuka kifo cha Imam Ja'far as-Swadiq (as), Imam wa sita wa madhehebu ya Shia Ithna-Asheri, maombolezo ambayo yamefanyika katika Msikiti wa Zeinabiyah huko Istanbul.
Maombolezo hayo yameanza mara tu baada ya kuswaliwa swala za Maghrib na Ishaa. Wapiga picha wa televisheni ya taifa ya TRT pia wameshiriki katika maombolezo hayo na kuchukua picha za shughuli zilizofanyika huko.
Televisheni hiyo inatazamiwa kuandaa filamu maalumu kuhusu shughuli ambazo hufanywa na Mashia katika siku za maombolezo na idi nchini humo. 668051