IQNA

Kikao cha kumuenzi Bibi Fatma (as) mjini Istanbul

19:13 - October 04, 2010
Habari ID: 2006593
Kikao cha saba cha kumuenzi Bibi Fatma Zahra (as) binti wa Mtume Mtukufu (saw) kilifanyika mjini Istanbul Uturuki hapo siku ya Jumapili. Kikao hicho kimeandaliwa na Jumuiya ya Marafiki wa Bibi Fatma (as) katika Kituo cha Utamaduni cha Furat (FKM).
Kikao hicho kilianza kwa kusomwa Qur'ani Tukufu na kisha wageni waalikwa walipewa fursa ya kumzungumzia bibi huyo mtukufu na hasa maisha yake ya kidini na pia nafasi yake akiwa mama na mke mwema.
Wanafikra na wasomi mbalimbali wa Kiislamu walishiriki katika kikao hicho na kutoa mitazamo yao tofauti kuhusiana na sifa pamoja na nafasi muhimu aliyokuwa nayo Bibi Fatma katika kueneza Uislamu katika zama zake. Pia walichambua nafasi ya maisha yake ya mtu binafsi, kijamii na kidini.
Mwishoni mwa kikao hicho washiriki walizawadiwa vitabu vinavyozungumzia maisha ya Bibi Fatma (as) vilivyoandikwa na waandishi wanawake. 668064
captcha