Mashindano hayo yatafanyika chini ya usimamizi wa Kituo cha Upashaji Habari cha Kiislamu kikishirikiana na taasisi ya al Amin na shule ya Iqra katika mji wa Vancouver kwa shabaha ya kuwahamasisha watu kihifadhi kitabu kitakatifu cha Qur'ani.
Mashindano hayo yatafanyika katika awamu nane tofauti za kuhifadhi juzuu za Qur'ani Tukufu.
Majina ya watu wanaotaka kushiriki kwenye mashindano hayo yataanza kuandikishwa Disemba mwaka huu.
Mashindano ya 9 ya kuhifadhi Qur'ani ya Canada yalifanyika katika awamu mbili tu na washindi wa tatu wa kwanza walitunikiwa zawadi. 668335