IQNA

Chuo Kikuu cha Michigan, mwenyeji wa maonyesho ya Qur'an Tukufu

17:04 - October 05, 2010
Habari ID: 2007222
Maonyesho ya Qur'ani Tukufu yameandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Greater Lansing katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Michigan nchini Marekani tokea Ijumaa ya tarehe Mosi Oktoba.
Kwa mujibu wa tovuti ya State news maonyesho hayo yameandaliwa na wakuu wa Kituo cha Kiislamu cha Greater Lansing katika kujibu dharau iliyofanyiwa Qur'ani Tukufu katika siku za hivi karibuni nchini Marekani.
Moja ya nuskha za Qur'ani zinazoonyeshwa katika maonyesho hayo ni ile iliyoandikwa katika karne za mwanzoni za Hijria. Vitabu vya kaligrafia ya Kiislamu, vinavyohusiana na Waislamu, na vinavyozungumzia suala la kuvumiliana kidini na kuchomwa moto vitabu vya mbinguni ni vinaonyeshwa pia katika maonyesho hayo.
Yassir Sardar mmoja wa wakuu wa Kituo cha Kiislamu cha Lansing amesema kuwa sababu ya kutolewa nuskha kadhaa za Qur'ani kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Michigan ni kushajiisha watu wasome na kukifahamu kitabu hicho ili kuzuia kutokea nchini Marekani vitendo vya dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu kama kile kilichoshuhudiwa hivi karibuni nchini humo ambapo Qur'ani Tukufu ilichanwa na kuchomwa moto.
Sardar pia amesema Kituo cha Kiislamu cha Lansing kina lengo la kuwagawia bure Wamarekani Qur'ani ili wapate kuijua zaidi.
Maonyesho hayo yataendelea kwa muda wa mwezi mmoja hadi tarehe 31 Oktoba. 668686
captcha