Taarifa iliyotolewa na ISESCO imesema kuwa mashambulizi ya walowezi wa Kiyahudi dhidi ya msikiti ni ukiukaji wa uhuru w kujieleza na kuvunjia heshima matukufu ya kidini.
Imesema kuwa hatua kama hizo ni kielelezo kamili cha ukiukaji wa sheria za kimataifa.
Taarifa ya ISESCO imesema kuwa walowezi wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza ni hatari kubwa kwa wananchi wa Palestina. Imesisitiza kuwa matukio hayo yote yanaonyesha tena kwamba kuwepo kwa vitongoji vya walowezi wa Kiyuzani katika eneo hilo ni kinyume na sheria za kimataifa.
Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo, shirika la ISESCO imesema kuwa vitendo vya Walowezi wa Kizayuni vya kuchoma moto misikiti na kuvunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur’ani ni ishara ya ukatili wa makundi ya Wazayuni dhidi ya wananchi wanaokandamizwa wa Palestina.
Mwishoni mwa taarifa hiyo Shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la nchi za Kiislamu limezitaka taasisi zote za kimataifa kulaani vikali kitendo hicho na kuwachukulia hatua watu waliotekeleza uhalifu huo. Vilevile ISESCO imezitaja jumuiya za kimataifa kuafiki suala la kuundwa dola huru la Palestina mji mkuu wake ukiwa Baitul Muqaddas. 669401