IQNA

Changamoto za uwekezaji wa Kiislamu kuchunguzwa nchini Qatar

14:33 - October 06, 2010
Habari ID: 2007787
Kikao cha kwanza cha kimataifa cha masuala ya uchumi wa Kiislamu kitaandaliwa huko Doha mji mkuu wa Qatar tarehe 20 na 21 kwa madhumuni ya kuchunguza changamoto na vikwazo vinavyoukabili uwekezaji wa Kiislamu.
Kuarifishwa uawekezaji wa Kiislamu kuwa chaguo bora la kuchukua nafasi ya uwekezaji wa jadi, kuimarishwa ushirikiano wa taasisi za fedha za Kiislamu kwa lengo la kuanzisha mfumo imara wa fedha katika kukabiliana na changamoto za serikali na kuainishwa majukumu ya kimaadili na kijamii ya uwekezaji wa Kiislamu ni malengo mengine ya kuandaliwa kikao hicho cha kimatifa.
Kikao hicho kitafanyika katika kivuli cha mihimili minne muhimu ambayo ni uchumi wa Kiislamu na uchumi wa nchi za Kiislamu, uchumi wa Kiislamu na matukio ya kiuchumi ya kimataifa, Taasisi za kifedha za Kiislamu na changamoto za serikali na hatimaye uwekezaji wa Kiislamu na majukumu ya kimaadili na kijamii.
Wataalamu na wawakilishi wa taasisi muhimu za uwekezaji kutoka nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu watashiriki katika kikao hicho. 668931
captcha