Kwa mujibu wa tovuti ya Express Buzz, kikao hicho kimefanyika kwa madhumuni ya kuufahamu vyema mfumo wa benki za Kiislamu.
Kutolewa huduma za Kiislamu nchini India ni maudhui kuu iliyojadiliwa na wawakilishi wa benki, wasimamizi wa mashirika ya bima, mashirika ya biashara, ofisi za biashara, viwanda, mashirika ya fedha na wahadhiri wa vyuo vikuu katika kikao hicho.
Akihutubia kikao hicho, Krishna Air, jaji wa zamani wa Mahakama Kuu ya India amesema kuwa mfumo wa benki za Kiislamu ambao unakataza riba umejengeka katika msingi wa thamani za kiutu na kwamba misimamo yote isiyofaa inayochukuliwa dhidi ya mfumo huo inapasa kufutwa. Amesema mfumo wa benki za Kiislamu unahimiza uzalishaji zaidi na kwamba jambo hilo linapelekea wanadamu kuwa na maisha bora zaidi.
Wazungumzaji wengine katika kikao hicho walisema kuwa mfumo wa kifedha wa Kiislamu si kwa manufaa ya nchi za Kiislamu pekee bali unazinufaisha nchi zote duniani. 669110