Baraza hilo limesema kuwa kitendo cha Mfaransa huyo hakikubaliki kabisa na kuelezea masikitiko yake makubwa kuwa kitendo hicho kumefanyika nchini humo.
Taarifa hiyo imesema kitendo hicho kwa hakika ni wito wa kushajiishwa ubaguzi wa rangi na ghasia za kidini jambo ambalo linakwenda kinyume na thamani za Ufaransa.
Baraza hilo la Waislamu limeendelea kusema kuwa kitendo hicho kwa hakika kitachochea mifarakano ya kidini na kuvuruga umoja wa raia wa Ufaransa. Limesema, katika siku za hivi karibuni limepokea picha za kukosewa heshima Qur'ani Tukufu kutoka kwa waovu wanaohusika na vitendo hivyo vya dharau na kuwataka Waislamu kuwa waangalifu na watulivu mbele ya vitendo kama hivyo vya kichochezi.
Mahakama moja ya Strasbourg imesema itamuhukumu mhalifu huyo ambaye anasemekana kuwa na umri wa miaka 30 kwa makosa ya kuvuruga utulivu wa umma na kuchochea ghasia. 669367