IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur’ani nchini Rwanda wazawadiwa

18:59 - October 06, 2010
Habari ID: 2007990
Washindi wa mashindano ya kuhifadhi na kusoma Qur’ani nchini Rwanda walienziwa na kuzawadiwa katika sherehe iliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Kigali.
Mashindano hayo yalisimamiwa na Wakala wa Waislamu wa Afrika (AMA) katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Watu 27 walichuana katika mashindano hayo, na tisa miongoni mwao walitambuliwa washindi. Washindi hao walitunukiwa zawadi zenye zaidi ya thamani ya franga milioni moja za Rwanda.
Mshindi wa kwanza alikuwa karii mwenye umri wa miaka 9 kwa jina la Abdullah Kyusa ambaye ataiwakilisha Rwanda katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Dubai.
Mufti wa Rwanda Sheikh Saleh Habimana alihutubia sherehe hizo akiwapongeza washindi wa mashindano hayo na kusisitiza kuwa ni jambo la dharura kwa Waislamu wote kujifunza Qur’ani kwa sababu kitabu hicho ndio marejeo ya kielimu ya Waislamu wote.
Mashindano ya Qur’ani ya Rwanda hufanyika kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa shabaha ya kushajiisha Waislamu kuhifadhi na kuelewa maana ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu. 669727

captcha