IQNA

Pendekezo la kuundwa Baraza la Maji la Kiislamu

14:07 - October 07, 2010
Habari ID: 2008209
Akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Mazingira wa Nchi za Kiislamu mjini Tunis, Rais Zainul Abideen bin Ali wa Tunisia ametoa pendekezo la kubuniwa Baraza la Maji la Kiislamu.
Amesema kuna uadharura wa kubuniwa baraza hilo kwa lengo la kutoa ushauri na kuwasilisha njia za kielimu za kukabiliana na matatizo ya maji na vilevile kupambana na ueneaji wa majangwa katika nchi za Kiislamu.
Amesema, kubuniwa njia za kuzuia israfu ya maji, usafishaji maji na kulindwa maji yaliyoko kwenye ardhi ni changamoto kubwa inayozikabili nch za Kiislamu hii leo, na kwamba kubuniwa baraza la maji litakalokuwa chini ya Jumuiya ya Nchi za Kiislamu linaweza kuwa suluhisho bora la tatizo hilo.
Amesema nchi za Kiafrika zinazidi kukabiliwa na ongezeka la jangwa jambo linalotishia mazao ya kilimo na hivyo kuhatarisha zaidi hali ya usalama wa chakula kwa watu wa bara hilo. 669830
captcha