IQNA

Ujumbe wa Iran watembelea Taasisi ya Qur’ani na Hadithi ya Rawalpindi

14:31 - October 07, 2010
Habari ID: 2008243
Ujumbe wa chuo cha kidini cha Qum Iran umetembelea Taasisi ya Qur’ani na Hadithi ya Rawalpindi nchini Pakistan na kukagua kwa karibu shughuli zinazofanyika katika kituo hicho cha Kiislamu.
Ujumbe huo ambao umekwenda Pakistan kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko uliongozwa na Nkurugenzi wa Taasisi ya Imam Khomeini Hujjatul Islam Hashimiyan.
Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na makari na mahafidhi wa Qur’ani kimesisitiza juu ya udharura wa kueneza mafundisho ya Qur’ani na hadithi.
Mwakilishi wa Jamiatul Mustafa al Alamiyya nchini Pakistan Abrar Hussein alitoa ripoti kuhusu utendaji wa ofisi ya taasisi hiyo.
Vilevile Mkurugenzi wa Tasisi ya Qur’ani na Hadithi ya al Zahraa Bibi Siddiq Alawi alizungumza machache kuhusu shughuli za taasisi hiyo.
669887
captcha