Mkurugenzi wa maonyesho hayo Mahdi Salim amesema kuwa maonyesho hayo yanafunguliwa jioni ya leo yakihudhuriwa na Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Ecuador na wawakilishi wa nchi zinazoshiriki katika maonyesho hayo.
Amesema nchi 30 zikiwemo Argentina, Uzbekistan, Marekani, Afghanistan, Uingereza, Sri Lanka, Russia, Indonesia, Palestina, Canada, Kenya, Cuba, India, Iraq, Syria na Tanzania zinashiriki katika maonyesho hayo. Nchi zinazoshiriki katika maonyesho hayo zinaonyesha bidhaa na uwezo wa vyombo vyao vya habari.
Mahdi Salim amesema kuwa mashirika mengi anayoshiriki katika maonyesho hayo ni ya Kiislamu na yanaonyesha bidhaa kama katuni na michezo na programu za kumpyuta.
Maonyesho ya Kimataifa ya Vyombo vya Habari vya Digitali yataendelea hapa mjini Tehran hadi tarehe 16 Oktoba. 670587