Kwa mujibu wa tovuti ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO, kikao hicho kitafanyika kwa uwenyekiti wa Rais Abdoulaye Wade wa nchi hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa hivi sasa wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC.
Kikao hicho kitafanyika pambizoni mwa awamu ya tisa ya mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Habari na Masuala ya Kiutamaduni COMIAC.
Mbali na kuchunguza masuala na matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu, kikao hicho kitachunguza pia sehemu ya kufanyikia mkutao wa wanafikra wa Kiislamu mwaka 2011 na jinsi ya kudhamini gharama za kikao hicho.
Muhammad al-Ghamari, mkuu wa kitengo cha uhusiano wa kigeni na ushirikiano cha shirika la ISESCO anashiriki katika kikao hicho kama mwakilishi wa shirika hilo. 670419