IQNA

Redio ya Qur'ani ya Misri, redio iliyo na wasikilizaji wengi zaidi

16:52 - October 10, 2010
Habari ID: 2010097
Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa na Muungano wa Redio na Televisheni wa Misri, Redio ya Qur'ani ya nchi hiyo ndiyo iliyo na wasikilizaji wengi zaidi nchini humo.
Kwa mujibu wa gazeti la Misri la Yaumu as-Saabi' Ibrahim Mujahid mkuu wa Muungano wa Redio na Televisheni za Misri ameashiria jambo hilo na kuongeza kwamba kutokana na matokeo ya uchanguzi huo wa maoni ambao ulisimamiwa na wataalamu husika, Redio Qur'ani ya Misri inasikilizwa na asilimia 98 ya wananchi wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, redio ya Ratiba ya Umma na ya Vijana na Michezo zinachukua nafasi za pili na tatu katika kuwavutia wasikilizaji. 670799
captcha