Akizungumza katika kikao cha ufunguzi cha mkutano wa kimataifa wa Sira ya Mtume Mtukufu (saw), Mufti Jumua amesema kuwa maisha ya Mtume Mtukufu (saw) yalikuwa na baraka kubwa kwa umma wa Kiislamu na hasa katika nyanja za subira na ukakamavu katika kipindi cha kulingania dini mjini Makka, mshikamano na maisha ya amani na wanadamu wengine katika kipindi cha kuhajiri Waislamu nchini Uhabeshi, kuwasaidia wanadamu wenzake katika jamii alipokuwa mjini Madina na kutekeleza uadilifu na kuwa na uhusiano mzuri na watu pamoja na wafuasi wa dini nyingine hasa mjini Madina.
Mufti wa Misri amesisitiza kwamba kila Muislamu anapasa kuzingatia masuala hayo manne maishani kwa sababu yanahusiana na kiumbe bora zaidi wa Mwenyezi Mungu duniani.
Ameongeza kuwa kufuata maisha ya Bwana Mtume kunamdhaminia mwanadamu saada na maendeleo humu duniani.
Kikao hicho cha siku mbili ambacho kimewajumuisha wanafikra, wanazuoni na wasomi wa Kiislamu kilianza siku ya Jumamosi.