Tovuti hiyo ndiyo itakayokuwa kubwa zaidi ya usomaji Qur'ani kwa njia ya intaneti nchini humo. Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharq, tovuti hiyo imezinduliwa kwa ushirikiano wa idara ya uhubiri na mwongozo wa kidini ya Wizara ya Wakfu ya Qatar na tovuti ya Islamweb.
Kundi la wataalamu wa teknolojia ya kumpyuta na masuala ya sheria za Kiislamu litasimamia tovuti hiyo ya Qur'ani.
Wasiamamizi wa tovuti hiyo wanasema kuwa huduma zilizowekwa kwenye tovuti hiyo zitawawezesha makumi ya mamilioni ya watu kote ulimwenguni kunufaika na kitabu hicho kitakatifu. 673409