Mkuu wa Taasisi ya Kielimu na Kiutamaduni ya al-Hadith amesema katika kikao cha nne cha kimataifa cha Muungano wa Idhaa na Televisheni za Kiislamu mjini Tehran kwamba vyombo vya habari vya ulimwengu wa Kiislamu vinapasa kutetea haki kwa kila njia na kwamba iwapo jambo hilo litathibiti, hali ya ulimwengu wa Kiislamu itabadilika kabisa.
Hayo yamesemwa na Ayatullah Muhamadi Reishahri, Mkuu wa Taasisi ya Kielimu na Kiutamaduni ya Dar al-hadith ambaye ameongeza kwamba nara ya mwaka huu ya kikao hicho ni muhimu sana kwa sababu iwapo itatekelezwa katika shughuli za vyombo vya habari vya Kiislamu, ni wazi kuwa si hali ya ulimwengu wa Kiislamu tu bali dunia nzima itabadilika. Amesema, umuhimu wa kubainishwa haki unadhihiri wazi tunapozingatia kwamba Qur'ani Tukufu imezungumzia neno hilo katika sehemu nyingi.
Amesema, kubainishwa haki ni jambo muhimu katika jamii na kwamba maana halisi ya Uislamu ni kuwa dini hii ni neno la haki.
Katika sehemu nyingine ya hutuba yake, Ayatullah Reishahri ameashiria kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu nchini Marekani na kusema kuwa maadui walitumia kila mbinu kutoa pigo dhidi ya haki katika kitendo hichop cha jinai.
Amesema kwa kutilia maanani suala hilo, vyombo vya habari vya Kiislamu vinapasa kufanya juhudi kubwa za kufikia lengo lao la kupigania na kudhihirisha haki duniani. 673214