Masomo hayo yanalenga kutoa elimu ya mbinu za tafsiri ya Qur'ani Tukufu. Taasisi ya al Mahdi pia itaanzisha masomo ya kitabu cha Nahjul Balagha na misingi ya maadili bora katika mtazamo wa Ahulbait (as) kuanzia kesho Jumatano ambayo yataendelea hadi Ijumaa ya tarehe 22 Oktoba.
Vilevile masomo ya tajwidi ya Qur'ani yataanza Alkhamisi ijayo na kumalizika tarehe 23 Oktoba.
Taasisi ya al Mahdi iliasisiwa mwaka 1993 kwa lengo la kutoa elimu na maarifa ya Kiislamu na imekuwa ikijishughulisha na kuitisha mikutano na makongamano ya kielimu na kutoa masomo ya muda ya Kiislamu na Qur'ani Tukufu kwa Waislamu na wasiokuwa Waislamu. 673453