IQNA

Mapumziko ya Idul Adh'ha kwa shule za Cambridge nchini Marekani

13:40 - October 13, 2010
Habari ID: 2012023
Shule za mji wa Cambridge katika jimbo la Massachusetts nchini Marekani kuanzia mwaka ujao wa masomo zitakuwa zikifungwa kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu ya Idul Adh'ha.
Kwa mujibu wa The Boston Channel, wakuu wa idara ya masomo ya jimbo la Massachusetts wamesema kuwa hatua hiyo ambayo ni ya kwanza kutekelezwa katika jimbo hilo itaanza kutekelezwa rasmi mwaka ujao wa 2011.
Wamesema wamechukua hatua hiyo ili kuheshimu haki za wafuasi wa dini ya Kiislamu wanaoishi katika mji wa Cambridge kama wanavyofanyiwa wafuasi wa dini mbili nyingine kubwa katika mji huo za Wakristo na Mayahudi.
Wameongeza kuwa si haki kuheshimu siku za mapumziko za Wakristo na Mayahudi katika mji huo na wakati huohuo kuwapuuza Waislamu. 673746
captcha